2 Chronicles 1:3-8

3 aNaye Sulemani na kusanyiko lote wakakwea mpaka mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni, kwa kuwa huko ndiko Hema la Kukutania la Mungu lilipokuwa, ambalo Musa mtumishi wa Bwana alikuwa amelitengeneza huko jangwani. 4 bBasi Daudi alikuwa amelipandisha Sanduku la Mungu kutoka Kiriath-Yearimu mpaka mahali alipokuwa amepatengeneza kwa ajili yake, kwa sababu alikuwa amesimamisha hema kwa ajili ya hilo Sanduku huko Yerusalemu. 5 cLakini yale madhabahu ya shaba ambayo Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, alikuwa ametengeneza yalikuwa huko Gibeoni mbele ya Maskani ya Bwana Mwenyezi Mungu, hivyo Sulemani na kusanyiko lote walimtafuta Mungu huko. 6 dSulemani akapanda huko yalikokuwa madhabahu ya shaba mbele za Bwana katika Hema la Kukutania, na kutoa dhabihu 1,000 za sadaka za kuteketezwa juu yake.

7 eUsiku ule Mungu akamtokea Sulemani na kumwambia, “Omba lolote utakalo nikupe.”

8 fSulemani akamjibu Mungu, “Umemwonyesha baba yangu Daudi fadhili nyingi, nawe umeniweka niwe mfalme mahali pake.
Copyright information for SwhKC